Uwajibikaji wa Kijamiii

Sehemu ya kuwa kampuni yenye maadili ni kusaidia wengine na kufanya ulimwengu kuwa bora.

Mkakati wa CSR na sehemu za kuzingatia

Kuwa na maadili na kujali kumekita mizizi katika maadili na itikadi za Expressfxt, pia kupata "Expressfxt Way" yetu wenyewe. Katika Wajibu wa Shirika kwa Jamii tunalenga kuunda mbinu yetu wenyewe, na kuileta ili izingatie sehemu tofauti tunapoendelea.

Tuna fikra za muda mrefu na tunapendelea kusaidia moja kwa moja kwa kufanya kazi na mashirika ya mashinani. Tunapoweza, tunatumia teknolojia na uwezo wa kujitolea wa timu zetu ili kuongeza ufanisi na ufikiaji. Hatuogopi mawazo shupavu.

Tuna sehemu tatu za kuzingatia - Elimu, Mazingira na Dharura.

Elimu

Elimu ndiyo msingi wa mabadiliko ya muda mrefu. Ndiyo maana tunawekeza katika miradi katika nyanja mbalimbali za elimu, iwe ni kwa kutoa vifaa muhimu kwa shule za msingi au programu bora za ufadhili wa masomo.

Mazingira

Ulinzi wa mazingira haujawahi kuwa muhimu zaidi. Tungependa kusaidia kwa upande wetu. Miongoni mwa programu zingine, tumeanzisha miradi ya upandaji wa miti ambayo tutapanua katika miaka ijayo. Pia tunaangalia hatua zetu za kimazingira, na kushirikiana na NGO za wataalam ili kuhakikisha uendelevu wa muda mrefu.

Dharura

Kwa kuwa kampuni ya kibinafsi yenye ufikiaji wa kimataifa, tunaweza kuleta athari ya kweli na yenye ufanisi wakati wa migogoro ya ndani na ya kimataifa. Tumetoa michango mikubwa katika kupambana na janga la Covid-19, na pia mioto ya misitu huko Cyprus. Pia tunahusika katika juhudi za kibinadamu zinazohusiana na shughuli za misaada wakati wa majanga kote duniani.

Kupambana na Covid-19

Wakati janga lilipoibuka tuliahidi Euro milioni 1 kulikabili. Tulitoa mchango wa mashine za kusaidia kupumua, vifaa vya hospitali, na vifaa vya maabara - vyote ambavyo vilikuwa vinahitajika kwa haraka na huduma za afya.

Cheza video

Miradi mingine na kujitolea

Tumeanzisha miradi mingi zaidi tangu kuanza kwa juhudi zetu za CSR katika Expressfxt. Mfano mmoja ni mchango wa mbao nyeupe, nyeusi na laini kwa shule za Pointe Larue na Anse Aux Pins nchini Ushelisheli, hatua ambayo ilipelekea madarasa 17 kufunguliwa tena.

Pia tulifanya shughuli ya uhifadhi wa bahari ambazo ni pamoja na usafishaji wa ufuo, mapango na chini ya maji katika Cyprus, na tukaelekeza fikira kwenye uhifadhi wa sili-watawa wa Mediterania kwa ufadhili wa video ya kuelimisha.

Mnamo 2022, wafanyakazi wetu walijitolea kwa masaa 676 katika miradi yetu ya CSR. Kilo 678 za takataka zilikusanywa, miti 280 ilipandwa katika juhudi za upandaji miti, na zaidi ya milo 6,000 ilitayarishwa kwa ajili ya misaada ya maafa.

Kufanya biashara kuna jukumu na fursa ya kuleta matokeo chanya ulimwenguni. Tunafurahia kusaidia wengine.”

Petr Valov Afisa Mkuu Mtendaji